MWANAMKE NI NANI
Mwenyezi Mungu akaumba mtu kwa mfano wake(mwanzo 1:27), kwa mfano wa Mungu alimwumba,mwanaume na mwanamke aliwaumba. Sisi wanawake ni watu wenye nguvu na ushawishi mkubwa katika kufanya mambo mengi kuliko wanaume. Endapo tutafanya mambo kwa kusudi la MunguTutambue tuliumbwa wanawake si kwa bahati mbaya bali Mungu alikuwa na kusudi jema la kutuumba na kutuweka katika ulimwengu huu, kwa hiyo tuamini nafasi yetu kama wanawake ni ya Muhimu mahali popote pale,sisi ni kama chumvi, na chakula kikikosa chumvi kinakuwa akina ladhaBwana alikuwa ameumba tayari wanyama , lakini mwanaume hakuwa na mwenza,alikuwa peke yake.Katika ubavu wa mwanamme Mungu akamtolea mwanamke .Mwanaume akamtambua mwanamke kama nyama yake