Monday, 12 June 2017

MIMI MWANAWAKE NAJITAMBUAJE


MWANAMKE NI NANI

 Mwenyezi Mungu akaumba mtu kwa mfano wake(mwanzo 1:27), kwa mfano wa Mungu alimwumba,mwanaume na mwanamke aliwaumba. Sisi wanawake ni watu wenye nguvu na ushawishi mkubwa katika kufanya mambo mengi kuliko wanaume. Endapo tutafanya mambo kwa kusudi la MunguTutambue tuliumbwa wanawake si kwa bahati mbaya bali Mungu alikuwa na kusudi jema la kutuumba na kutuweka katika ulimwengu huu, kwa hiyo tuamini nafasi yetu kama wanawake ni ya Muhimu mahali popote pale,sisi ni kama chumvi, na chakula kikikosa chumvi kinakuwa akina ladhaBwana alikuwa ameumba tayari wanyama , lakini mwanaume hakuwa na mwenza,alikuwa peke yake.Katika ubavu wa mwanamme Mungu akamtolea mwanamke .Mwanaume akamtambua mwanamke kama nyama yake
Wanawake ni Furaha

Kama wanawake tusisubiri tuwezeshwe inatakiwa tujiwezeshe kwanza wenyewe, kujishughulisha katika shughuli mbalimbali ya kujiinua kiuchumi, kuwa washauri bora katika nchi , jamii na familia zetu, kama wanawake tunatakiwa tuongeze juhudi za ziada na nia ya mafanikio  katika mambo mbalimbali , Iwapo imetokea aneth au judith ameshindwa katika jambo fulani inaonekana wanawake ndo wameshindwa, hata jambo baya linapotokea akiwa amefanya mama au binti yoyote itajulikana ni mwanamke amekosea , yatupasa wanawake tuonyesha picha nzuri katika jamii yetu ili tutunzee thamani yetu.

Wednesday, 28 January 2015

MAMBO AMBAYO MWANAMKE MWENYE UPENDO WA KWELI HAKOSI






             Kama tunavojua wapendwa katika dunia ya sasa kumpata mwanamke mwenye upendo wa dhati ni vigumu, wengi wa wanawake huwa wapo kwa ajili ya pesa au kujishikiza ili mradi nae aonekane yupo na mtu, utakuta wanawake wazuri wengi wapo tena wanavutia na pia wana maumbo mazuri lakini huishia kama chombo cha starehe tu ambapo hawaolewi kutokana na kutokukizi tabia zinazofaa, kuwa na viburi na kujiona wao ndio wao.Utakuta wanawake wengi wanaingia gharama san ya kujiremba na vipodozi kibao, kununua nguo za mitego, kuongeza maumbo wakiamini kuwa  yote hayo wataweza kupata mme wa kuvutiwa nao ili waolewe.kama wanwake inabidi tujitambue na kama tuna nia ya kuingia katika ndoa tunatakiwa tuwe na silaha ya tabia njema.

Yafuatayo ni mambo muhimu ya kuweza kumtambua mwanamke bora na mwe upendo wa dhati:-

Daima ni muaminifu na anaaminika sana kwa matendo yake
Msikivu na mtii 
Mwanamke mvumilivu
Anaependa na kujali ndugu zako.
Mshauri wako wa kwanza .
Ana hekima katika kuyakabili mambo mbalimbali. hata siku moja haamui mambo kwa ujinga na daima busara yake ndio silaha yake .
Huwa mwepesi wa kukiri makosa yake na kuomba samahani.
Ni mcha Mungu, kwa imani yake.
Si mpayukaji wala mtu wa kisirani . maneno yake huwa yaliyopangiliwa kwa sauti yenye kunyesha mamlaka lakini yenye upole.
Kamwe huwa hana dharau, wala majivuno, wala kiburi, wala uchoyo wala unafiki kwa mtu yeyote yule.
Mwenye heshima
Mwenye mvuto.
Anayejiamini.
Mwenye utu na anayemthamini mme wake au mchumba wake.
Anayetunza siri.
Anayejipenda na msafi
Mchapakazi
Mwenye kuleta furaha.
Mbunifu.
Mvumilivu,

Ukipata mwanamke mwenye tabia njema umepata dhahabu,ni hayo tu

Nawatakia siku njema
 

MIMI MWANAWAKE NAJITAMBUAJE

MWANAMKE NI NANI  Mwenyezi Mungu akaumba mtu kwa mfano wake(mwanzo 1:27), kwa mfano wa Mungu alimwumba,mwanaume na mwanamke aliwaumba. ...